Inakuja hivi karibuni
Biashara Yako Mfukoni Mwako
App ya Biashara Sauti kwa simu za Android inakuja hivi karibuni kwenye Google Play - salama kupakua, na inajisasisha yenyewe. Usisubiri: anza leo kwenye kivinjari cha simu yako, na app ikitoka ingia tu kwa namba yako - kila kitu kitakuwepo.
Itakavyokusaidia
Akaunti moja, kwenye simu, kompyuta na simu za wafanyakazi.
Inafanya kazi bila internet
Duka lako ndani ya simuBando likiisha au mtandao ukikatika, kazi inaendelea. Kila kitu kinatumwa chenyewe mtandao ukirudi.
- Uza, rekodi madeni na matumizi bila internet
- Ongeza na hariri bidhaa na stoo
- Ripoti na Sauti ya Biashara kwenye simu
- Simu mbili zikiuza bidhaa ile ile, mfumo unakuambia uhesabu stoo
Akaunti moja kila mahali
Namba ya simu na nenosiriIngia kwa namba yako ya simu na nenosiri - kwenye app, kwenye kompyuta au kivinjari. Taarifa ni zile zile.
- Jisajili ndani ya app au kwenye tovuti
- Simu mpya inathibitishwa kwa SMS mara moja tu
- Wafanyakazi wanaingia kwa namba zao wenyewe
- Siku 7 za kujaribu bure
Anza Leo, Bila Kusubiri
Kila unachofanya sasa kitakuwepo kwenye app ikitoka.
- Fungua biasharasauti.com kwenye kivinjari cha simu yako (Chrome).
- Jisajili kwa jina, namba ya simu na nenosiri, kisha weka namba ya SMS.
- Weka taarifa za biashara yako na anza kurekodi mauzo.
- App ikitoka Google Play, ipakue na uingie kwa namba ile ile.
Kwa usalama wako, pakua app ya Biashara Sauti kutoka Google Play pekee itakapotoka - usisakinishe faili za app (APK) unazotumiwa na mtu mwingine. Maswali? WhatsApp.
