Mifuko ya Pesa
Cash, M-Pesa, benki au Mkopo - jua kila shilingi iliingia wapi.
Rekodi mauzo, stoo na matumizi - mfumo unakuambia nini cha kufanya leo ili kuongeza faida.
App ya Android inakuja hivi karibuni kwenye Google Play. Itafanya kazi hata bila internet
Duka, genge, saluni au hardware - rekodi kila mauzo kwa kugusa mara moja, kwa Kiswahili au Kiingereza.
Inasoma mauzo, stoo, matumizi na madeni yako, kisha inakuambia nini cha kufanya leo.
Mfumo umejengwa kwa ajili ya kazi za kila siku za duka - rahisi, haraka na wazi.
Cash, M-Pesa, benki au Mkopo - jua kila shilingi iliingia wapi.
Mauzo, faida na matumizi kwa siku, wiki au mwezi - kwa michoro rahisi.
Stoo inapungua yenyewe kila mauzo, na unajua kinachokaribia kuisha.
Mfumo kamili wa kusimamia duka lako.
Fuatilia nani anadaiwa, kiasi gani na tangu lini - hata akilipa kidogo kidogo.
Umeme, nauli, kodi, mishahara - ona pesa inaenda wapi kila mwezi.
Mteja analipia kwanza kidogo kidogo; bidhaa zinahifadhiwa hadi amalize.
Kila mfanyakazi anaingia kwa namba yake ya simu; cheo chake kinaamua anachoona - faida na ripoti zinabaki kwako.
Simamia matawi yako yote mahali pamoja na hamisha stoo kati yao.
Tunaiweka kwenye Google Play ili uipakue kwa usalama na ipate masasisho yenyewe. Itakuwa na:
Jina, namba ya simu na nenosiri - chini ya dakika 2.
Tunakutumia SMS yenye namba ya uthibitisho.
Jina la duka na mahali - kisha anza kuuza, siku 7 bure.
Siku 7 zikiisha, chagua kifurushi, lipa kwa simu, kisha tupigie au tuandikie WhatsApp. Tunaiwasha papo hapo.
Anza na siku 7 bure, bila kulipa chochote. Ukiridhika, chagua kifurushi kinachokufaa.
Kifurushi kimoja chenye kila kitu cha kuendesha biashara yako.
Lipa mwezi kwa mwezi. Acha wakati wowote.
Sawa na 12,500 TZS kwa mwezi · miezi 2 bure
Anza siku 7 bureHakuna malipo ili kuanza · Acha wakati wowote
Lipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au benki, kisha tupigie au tuandikie WhatsApp. Tunaiwasha biashara yako tukishaona malipo. Huhitaji namba ya muamala.
Biashara inasimama hadi uchague kifurushi na kulipia. Taarifa zako zote zinabaki salama na zinarudi kama zilivyo.
Ndiyo. Tunazihifadhi siku 90 baada ya kifurushi kuisha, na tunakutumia SMS mbili kabla ya kuzifuta.
Hapana. Kifurushi kimoja kinalipia biashara yako na matawi yake yote. Biashara nyingine tofauti ina kifurushi chake.
Ndiyo. Siku zilizobaki hazipotei, kipindi kipya kinaanza kile cha sasa kikiisha.
Ndiyo. Siku 7 bila malipo yoyote, mara moja kwa kila namba ya simu.
Chini ya dakika 2: jina, namba ya simu na nenosiri. Utapokea SMS ya uthibitisho.
Fungua akaunti kwa namba yako ya simu, kisha weka jina la biashara yako na mahali ilipo.